Vita dhidi ya Ebola vyakwamisha jamii kijijini Sierra Leone

Vita dhidi ya Ebola vyakwamisha jamii kijijini Sierra Leone

Pakua

Baada ya visa 25 vya Ebola kuibuka kwenye kijiji cha Aberdeen, nchini Sierra Leone, kijiji kizima kimewekwa kwenye karantini.

Watalaam wa afya wa serikali ya Sierra Leone, mashirika yasiyo ya kiserikali na wafanyakazi wa kijamii wanafuatilia waliokua karibu na magonjwa ili kukomesha mlipuko kwenye eneo hilo.

Lakini, wakati huo huo, shughuli zote za uchumi zimekwama, mathalani wavuvi hawawezi tena kwenda kuvua samaki. Kulikoni? Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.

Photo Credit
Picha kutoka UNIFEED. Mwanamke huyu amewekwa karantini, kwenye kijiji cha Aberdeen.