Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Tanzania inapaswa kuchukua hatua ili kutokomeza mauaji dhidi ya albino

Serikali ya Tanzania inapaswa kuchukua hatua ili kutokomeza mauaji dhidi ya albino

Pakua

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora Tanzania, Tom Bahame Nyanduga, amesema ni jukumu la serikali kuhakikisha kwamba watekelezaji wa mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi wanapewa adhabu kali itakayozuia wengine kujiingiza kwenye vitendo hivyo vya kinyama. Ameongeza kwamba serikali ya Tanzania inapaswa kuwapatia watu hao, hasa watoto, ulinzi wa kutosha. Aidha amesema ni lazima jamii ielimishwe ili kutokomeza unyanyapaa dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi au albino.

Katika mahojiano na Priscilla Lecomte, Nyanduga ameanza kwa kulaani vikali mashambulizi yaliyotokea siku chache zilizopita dhidi ya Yohana Bahati, mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja aliyeteswa na kuuawa kwa msingi wa ulemavu wake wa ngozi.

Photo Credit
Picha ya IRIN/Helen Blakesley