Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tupunguze kiwango cha mlo kadri jua lizamavyo: Mtaalamu akizungumzia Kisukari

Tupunguze kiwango cha mlo kadri jua lizamavyo: Mtaalamu akizungumzia Kisukari

Pakua

Tarehe 14 mwezi Novemba kila mwaka ni siku ya kisukari duniani. Siku hii ni Ikiwamahsusi kutathmini mwelekeo wa matibabu dhidi ya ugonjwa huo wenye aina mbili; Kisukari aina ya kwanza ambayo ni ya kurithi na aina ya pili inayotokana na mwili kushindwa kutumia vizuri kichocheo cha Insulin. Ujumbe wa mwaka huu ni maisha yenye afya na kisukari. Shirika la Afya duniani, WHO linasema kuwa zamani ugonjwa wa kisukari ulionekana ni kwa ajili ya jamii zenye uwezo lakini hivi sasa ugonjwa huo umejikita nchi maskini kichocheo zaidi kikiwa ni utipwatipwa au unene wa kupindukia. Mathalani asilimia 80 ya vifo takribani Milioni Moja na Nusu vilivyotokea duniani kote mwaka 2012 kutokana na Kisukari ni katika nchi za vipato vya kati na chini. Na zaidi ya hayo WHO inasema aghalabu huchukua muda kwa mtu kugundua ana Kisukari. Je hali ya Kisukari iko vipi huko Afrika Mashariki, na mlo gani ni sahihi? Basi tuanzie huko Mwanza Tanzania ambako Martin Nyoni wa Radio washirika Radio Saut amevinjari hospitali ya rufaa ya Bugando.

Photo Credit
Evelyne Musera mgonjwa wa Kisukari kutoka Kenya. (Picha-WHO)