Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utafiti si kuandika vitabu, ni kuleta faida kwa watu: KMFRI

Utafiti si kuandika vitabu, ni kuleta faida kwa watu: KMFRI

Pakua

Taasisi ya Utafiti wa Samaki za Bahari (KMFRI) nchini Kenya. Pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo FAO na wadau wengine wamebuni teknolojia mpya ya kuwezesha wavuvi kupata taarifa kuhusu bei ya samaki kwenye soko kupitia simu za mkononi.

Teknolojia hiyo baada ya kubadilisha maisha ya watu nchini Kenya, sasa inapelekewa nchini Uganda mwezi huu ambapo katika mahojiano na idhaa hii, Dkt. William Oweke Ojwang mtaalam kutoka KMFRI amesema mfumo huo utaleta faida kwa wavuvi wadogo wadogo, wafanyabiashara na hata viwanda vya samaki kwani kwa maoni yake utafiti haumaanishi kuandika vitabu bali pia kusaidia watu.

Photo Credit
Picha kutoka video ya mradi wa Smart Fish / FAO