Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uandikishaji sawa kati ya wasichana na wavulana katika shule ya msingi na ya sekondari waangaziwa, Tanzania

Uandikishaji sawa kati ya wasichana na wavulana katika shule ya msingi na ya sekondari waangaziwa, Tanzania

Pakua

Lengo la tatu la maendeleao ya  milenia ni kuimarisha usawa wa kijinsia na kustawisha wanawake. Katika kufikia lengo hili suala kuu ni kuimarisha uandikishaji sawa kati ya wasichana na wavulana katika shule ya mzingi na vile vile shule ya sekondari kabla ya mwaka 2015.

Kwa ujumla dunia imefikia kawa kiasi usawa wa kutoa elimu kwa wasichana kwa wavulana lakini ni nchi chache tu ambazo zimefikia lengo kwa asilimia mia moja katika ngazi zote za elimu.

Katika baadhi ya nchi hususan zile za kipato cha chini upatikanaji wa elimu kwa wote ni jambo ambalo bado linakabiliwa na changamoto kutokana na umaskini.Tanzaniani moja ya mataifa 189 yaliyoridhia utekelezaji wa malengo ya milenia ifikapo mwaka 2015.

Wakati zikiwa zimesalia siku chache kukamilisha malengo hayo, hali ikoje nchini humo? basi ungana na Tamimu Adamu wa radio washirika Jogoo fm, Songea mkoaniRuvumaambapo alivinjari katika shule mbili kujionea hali halisi.

Photo Credit
Picha@UNICEF