EAC imepiga hatua utekelezaji malengo ya milenia:Eriyo

EAC imepiga hatua utekelezaji malengo ya milenia:Eriyo

Pakua

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Jessica Eriyo amesema kanda ya Afrika Mashariki inayojumuisha nchi 5 wanachama imepiga hatua muhimu kwenye utekelezaji wa malengo ya millennia.

Katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kando mwa kongamano la vijana wa Afrika Mashariki juu ya mabadiliko ya tabia nchi jijini Mwanza, Tanzania, Naibu katibu mkuu huyo amesema licha ya baadhi ya maeneo kutofanya vizuri, Afrika ya mashariki inachukua juhudi zaidi ili kukabiliana na mkwamo huo.

sehemu kubwa katika maeneo kama elimu, afya na maeneo mengine bado hatujapiga hatua ya kujivunia ila kusema kweli juhudi muhimu bado zinachukuliwa, na zinahitajika zaidi. kwa kutambua hilo nchi za afrika mashariki zinafanya kazi kikamilifu, ikihusisha nchi moja moja na juhudi za pamoja hasa zikilenga kutizama hatua mpya baada ya mwaka 2015” amesema Eriyo.

Eriyo pia ameainisha lengo la saba la millennia linalohimiza mazingira endelevu kama eneo linalozipeleka puta nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki huku akitaja ukosefu wa nishati ya kutosha kuwa kunaongeza mbinyo katika kukabiliana na uharibifu mazingira.

Katika hatua nyingine, Eriyo amewatolea wito viongozi wa kanda hiyo ya Afrika kutekeleza mipango ya maeneo ya vipaumbele ikiwa ni pamoja na kutumia rasimali zilizopo ili kutimiza malengo ya milennia.

Photo Credit
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Jesica Eriyo wakati wa mahojiano na Rashid Chilumba.Picha ya UM/Kiswahili/Richard Chilumba