Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Familia inachangia kujenga jamii: Hali ikoje Burundi?

Familia inachangia kujenga jamii: Hali ikoje Burundi?

Pakua

Tarehe 15 Mei ya kila mwaka ni siku ya familia duniani ambapo ujumbe wa mwaka huu umeangazia umuhimu wa kuimarisha familia ili kuweza kufikia malengo ya maendeleo ya milenia hususan lile la kutokomeza umaskini. Katika ujumbe wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema kuwa familia zina mchango mkubwa katika kujenga jamii inayowajibika. Hata hivyo mengi yanapaswa kufanywa ili familia ziweze kutimiza wajibu huo. Familia yenye uwezo inaweza kuhakikisha wanachama wake wote wanapata mlo wa kutosha, wanapata elimu bora na wanakuwa raia wanaowajibika vyema na ipasavyo kwa nchi yao na hivyo kufanya dunia pahala bora zaidi. Je nchini Burundi hali iliko vipi? Wananchi wanasemaje? Serikali nayo inachukua hatua gani? Basi ungana na mwandishi wetu wa maziwa makuu, Ramadhani Kibuga ambaye katika makala hii ya wiki anaanzia mtaa wa Buyenzi, kwenye mji mkuu Bujumbura.

Photo Credit
UN Photo/B Wolff