Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na kaulimbiu "Samaki safi, maisha bora"

FAO na kaulimbiu "Samaki safi, maisha bora"

Pakua

Uvuvi wa kupindukia ni moja ya tishio kubwa kwa utunzaji wa rasilimali za mabahari na usalama endelevu wa chakula. Shirika la chakula na Kilimo Duniani FAO limejadili changamoto hiyo katika kongamano la kimataifa kuhusu bahari na usalama wa chakula, lililofanyika The Hague, Uholanzi, kuanzia tarehe 24 hadi 25, April mwaka huu. Kwa mujibu wa FAO, ni muhimu kuelimisha jamii kuhusu uvuvi endelevu kwanzia ngazi ya wavuvi wadogo wadogo wanaochangia kwa kiasi kikubwa katika matumizi ya rasimali hiyo. Tayari FAO imeanza mradi wa kusimamia uvuvi endelevu kwenye maeneo ya Ziwa Victoria linalotumiwa na Kenya, Tanzania na Uganda. Basi kwa undani zaidi fuatana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii .

Tizama hapa filamu ya mradi huu