UNMISS yaunga mkono juhudi za kikanda za kurejesha amani Sudan Kusini

26 Disemba 2013

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa ujumbe wa UNMISS, Hilde Johnson, amewahutubia waandishi wa habari kwa njia ya video leo na kusema kuwa taifa la Sudan Kusini limetumbukia katika hali ya sintofahamu na kuyumbayumba, na kutoa wito kwa viongozi kuchukua hatua za dharura kurejesha utulivu.

Bi Johsnon ambaye amezuru kambi za watu walolazimika kuhama makwao leo, amesimulia baadhi ya visa vya matatizo wanayokumbana nayo raia wa Sudan Kusini, ikiwemo watoto kuzaliwa na kambini, huku wengine wakikumbana na hatari za mara kwa mara.

Amesema anasubiri matokeo ya mkutano wa IGAD mjini Nairobi kesho, baada ya ziara ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn mjini Juba hii leo

“Ujumbe wa UNMISS unaunga mkono kikamilifu juhudi hizi za kina na zinazoendelea za nchi jirani za Sudan Kusini katika kutafuta suluhu la amani kwa mzozo huu. Nimekuwa nikifanya mazungumzo na Rais Kiir na viongozi  wengine wa kisiasa wa Sudan Kusini na viongozi wa kijamii, kuhuru harakati hizi, ili kumaliza magigano na ghasia zinazoendelea sasa”

Bi Johnson pia amesema ujumbe wa UNMISS utaendelea kuwepo Sudan Kusini na kuwalinda raia, huku akisema sasa wanaendelea kupanua uwepo wao kote nchini, huku wakiwahamisha wafanyakazi wasio wa lazima kutoka maeneo Fulani.

“Hivi sasa tuna zaidi ya raia 50,000 kwenye kambi zetu Juba, Bor, Bentiu, Malakal na kwingineko. Na kuwapo kwao kwenye kambi hizi ni ushahidi dhahiri wa mahitaji makubwa ya kuongeza operesheni za Umoja wa Mataifa Sudan Kusini. Kwa hiyo, hatuondoko Sudan Kusini. Tutaendelea kuwepo hapa, na tupo hapa kulinda. Tutafanya kila kitu katika uwezo wetu, lakini pia tunahitaji kuongeza rasilmali zetu.”

Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu pia amelishukuru Baraza la Usalama, ambalo Jumanne wiki hii lilipitisha azimio la kuongeza uwezo wao, kwa kuidhinisha kuongeza idadi ya vikosi vya kulinda amani kwa wanajeshi wengine 5,500.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud