Hakuna vita vya wenyewe kwa wenyewe katika ugaidi bali vita dhidi ya ugaidi:Syria

30 Septemba 2013

Sera za fujo dhidi ya Syria ni hatua ya kwanza kuelekea kwenye suluhisho nchini humo kwa mujibu wa naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje Walid Al-Moualem.

Akizungumza kwenye mjadala wa baraza kuu Jumatatu amesema suluhu yoyote ya kisiasa wakati msaada kwa ugaidi iwe kwa kuwapa silaha, fedha au mafunzo ni kiini macho na upotoshaji.

(SAUTI YA WALID AL-MOUALEM)

“Syria imetangaza tena na tena kwamba inaafili suluhu ya kisiasa kwa mgogoro wake, sasa ni juu ya wale wanaodai kuunga mkono suluhu ya kisiasa Syria kukomesha vitendo vya machafuko na sera dhidi ya Syriana kwenda Geneva bila masharti. Kwa misingi ya haki za watu za kujitawala watu wa Syria wana mamlaka ya kuchagua uongozi wao, wawakilishi wao na kuamua mustakhbali na mfumo wa siasa ambao utajumuisha jamii nzima ya Syria ikiwemo walewaliorubuniwa na kusukumwa kufuata njia potofu”

Al-Moualem amesema hakuna vita vya wenyewe kwa wenyewe Syria , bali ni vita dhidi ya ugaidi ambao hautambui mila, haki wala usawa na kudharau haki zozote na sheria.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud