Hadhi ya ukimbizi kwa wanyarwanda kukoma mwisho wa mwezi huu: UNHCR

28 Juni 2013

Takribani wanyarwanda 100,000 wanaosihi uhamishoni huenda wakapoteza hadiyaoya ukimbizi ifikapo tarehe 30 mwezi huu kwa mujibu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

 (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Wale ambao watatambuliwa kuwa wakimbizi ni wale walioihama nchi kabla ya tarehe 31 mwezi Disemba mwaka 1998. UNHCR inasema kuwa mikataba ya kimataifa na muungano wa Afrika inasema kuwa hali ya kuwa mkimbizi inafikia kikomo mara kunapofanyika mabadilko kwenye nchi walikotoka wakimbizi  na ikiwa yale yaliyochangia wakimbizi hao kukimbia makwao hayapo tena. Msemaji wa UNHCR Adrian Edwards anasema kuwaRwandasasa ina amani ya kutosha hali ambayo imechangia wakimbizi miloni 3.5 walioikimbia nchi hiyo  wakati wa mauji ya kimbari mwaka 1994 kurudi nyumbani.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)

“Kuna wakimbizi 100,000 walio nje ya nchi. Ifikapo Jumapili hali ya kuwa mkimbizi itafikia kikomo. Na tena kile ambacho kimekuwa kikifanyika ni kuwashurutisha watu  kurudi kwa hiari  na pia kujaribu kuwahakikishia wenye wanahitaji usalama wa kimataifa kuwa wanaendelea kuupta. Lakini kwa kila hatua  hii ina maana kuwa asilimia kubwa watarudi nchini Rwanda. Wakimbizi wa Rwanda waliosalia wako nchini Burundi, Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.. Kenya , Malawi, Musumbiji. Congo , Afrika Kusini, Uganda, Zambia na Zimbabwe.”

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud