Mahiga alaani mauaji ya mwandishi wa habari mjini Mogadishu

25 Machi 2013

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia, Balozi Augustine Mahiga, ameshtushwa na kuhuzunishwa na mauaji ya mwandishi wa habari, Rahma Abdulkadir aliyekuwa akifanya kazi na Redio ya Abduwaq.

Watu wasiojulikana wanaripotiwa kumshambulia Bi Abdulkadir kwa bastola na kumuua katika mtaa wa Yaqshid, mjini Mogadishu.

Bwana Mahiga amekilaani vikali kitendo hicho, akisema kuwa Somalia inaendelea kuwa mahali pa hatari zaidi kwa waandishi wa habari, na kwamba picha hiyo ya hatari inatakiwa kubadilika.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud