WHO yabuni vyombo vya kuongeza mazingira salama katika hospitali za Afrika

31 Januari 2013

Shirika la Afya Duniani (WHO), leo limetoa fungu la vyombo vitakavyotumiwa kwa minajili ya kuboresha usalama wa wagonjwa hospitalini katika nchi zinazoendelea.

Fungu hilo la vyombo muhimu limebuniwa kwa ushirikiano wa wataalam wa afya kupitia mpango wa WHO wa ushirikiano wa African Partnerships for Patient Safety (APPS), ambao unaweka hospitali kumi na nne kutoka barani Afrika katika ushirikiano wa bega kwa bega kila moja na hospitali kutoka Uingereza, Ufaransa na Uswisi.

Kupitia kwa mpango huo, wataalam wa afya kutoka hospitali hizo zinazoshirikishwa barani Afrika na Ulaya, wamebuni njia za kushirikiana na kusaidiana kuweka mazingira salama kwa huduma za uuguzi. Kwa pamoja wamebuni njia ya kutumia vyombo vilivyoorodheshwa na WHO kwa matumizi ya upasuaji salama hasa katika mazingira ya hospitali zilizopo barani Afrika. Tarik Jasarevic ni msemaji wa WHO.

(SAUTI YA TARIK JASAREVIC)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud