Jumuiya ya kimataifa yaomba dola milioni 471 kwa ajili ya Afghanistan

28 Januari 2013

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema kuwa watoto 165 walio na umri wa chini ya miaka mitano wanakufa kila siku huku mama mjamzito mmoja akifariki dunia kila baada ya saa mbili nchini Afhanistan.

Taarifa hiyo ya OCHA inalenga kuonyesha jinsi hali ya kibinadamu inavyozidi kuzorota nchini Afghanistan.

Inaongeza kuwa wakati hali ya kibinadamu inapozidi kuwa mbaya hali mbaya ya usalama, mizozo, kuhama kwa karibu watu nusu milioni na kuongezeka kwa makazi duni mjini vyote vinachangia kudorora zaidi kwa hali iliyopo sasa.

Kulingana na Mark Bowden ambaye ni mratibu wa masuala ya kibinadamu ni kuwa kiasi hicho cha Doka Milioni 471 kwa mwaka huu kina lenga kutoa msaada kwa waliohama makwao ,na kuwapunguzia athari za majanga ya kiasili.

Anasema kuwa kati ya mikoa iliyo na mahitaji zaidi ni pamoja na Kandahar, Hilmand, Nangarhar, Ghazni na Kunar. Kulingana na OCHA ombi la mwaka 2012 lilifadhiliwa kwa asilimia 48 likiongeza kuwa linahitaji ufadhili zaidi mwaka huu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud