Mateka waliookolewa kurejeshwa nyumbani: UNPOS

2 Januari 2013

 Umoja wa Mataifa kwa sasa unaongoza shughuli ya kuwarudisha makwao mateka waliookolewa hivi kutoka kwa maharamia wa kisomali baada ya miaka mitatu mikononi mwa maharamia hao.

Mateka hao waliokolewa kufuatia oparesheni iliyochukua muda wa siku 15 iliyoongozwa na polisi wa baharini wa eneo la Puntland tarehe 23 mwezi Disemba mwaka uliopita. Mabaharia hao 24 ni wa meli ya MV Iceberg 1 iliyotekwa nyara mwezi Machi mwaka 2010 kwenye Ghuba ya Aden.

Mateka hao kisha walisafirishwa kwenda Nairobi kupitia mpango wa kuwahudumia mateka unaoongozwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNPOS kwa ushirikiano na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na madawa ya kulefya na uhalifu UNODC kabla ya kusafirishwa kwenda makwao.

Leonardo Hoy-Carrasco ni afisa kutoka ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud