Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba wa kimataifa juu ya haki za wafanyakazi za majumbani kuanza kufanya kazi mwakani:UM

Mkataba wa kimataifa juu ya haki za wafanyakazi za majumbani kuanza kufanya kazi mwakani:UM

Pakua

Mkataba wa Umoja wa Mataifa ambao unaangazia ustawi bora kwa wafanyakazi wa majumbani unatazamiwa kuanza kufanya kazi unaendelea kupata uungwaji mkono baada ya kuridhiwa na mmoja ya nchi wanachama.

Mkataba huo pindi utapoanza kufanya kazi rasmi unatazamia kuinua ustawi wa wafanyakazi wa majumbani zaidi ya milioni moja ambao kwa miaka mingi ustawi wao bado haujazingatiwa.

Tayari mamlaka ya Philippines imeridhia mkataba huo na hivyo kutoa ruksa kuanza kufanya kazi kuanzia mwaka ujao wa 2013. Mkataba huo wa kimataifa kwa ajili ya wafanyakazi wa majumbani unataka wafanya kazi kutambulika na kupewa haki zao zote kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine.

Mkataba huo uliasisi mwaka uliopita mjini Geneva kufuatia juhudi kubwa zilizoendeshwa na shirika la kazi duniani ILO, na ili mkataba huo uanze kufanya kazi kwanza unapaswa kuridhiwa na nchi wanachama.