Migiro asema kwaheri Umoja wa Mataifa

29 Juni 2012

Naibu Katubu Mkuu wa Umoja wa mataifa wiki hii anafungasha virago na kurejea nyumbani Afrika baada ya kuutmikia Umoja wa mataifa kwa miaka mitano.

Migiro ambaye ni mwanamke wa pili kushika wadhifa huo na kwanza barani Afrika anasema anaondoka Umoja wa Mataifa kifua mbele akijivunia mengi mazri na mafanikio aliyoyapata si kwake binafsi bali kwa nchi zote wanachama waliokwa wakitarajia mengi kutoka kwake.

Katika sehemu hii ya kwanza ya mazungumzo na Asha-Rose Migiro naibu Katibu tunamulika miaka mitano ya uongozi wake kwenye Umoja wa Mataifa. Asha-Rose anaondoka Umoja wa Mataifa akiwa amefanya mengi ya kukumbkwa.

Amekuwa chachu kwa wanawake wengine, amekuwa changamoto kwa wanaosema wanawake hawawezi na amekuwa mfano wa kuigwa kama mwanamke shupavu.

Aliteuliwa mwaka 2007 akiwa ni mwanamke wa pili kuwa naibu Katibu Mkuu katika historia ya Umoja wa mataifa.

Bi Migiro ameketi na mtangazi wa Idhaa hii Joshua mmali na kumweleza yaliyo moyoni mwake baada ya miaka mitano ya pilika nyingi. Tega sikio.

(MAHOJIANO NA BI ASHA ROSE MIGIRO)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud