WFP yaanzisha mpango wa vocha kusaidia Wazimbabwe wenye HIV

30 Aprili 2012

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeanzisha mpango wa ubunifu nchini Zimbabwe utakaosaidia kuwalisha walio katika shida na wengi wao ni wale wanaoishi na virusi vya HIV.

WFP inatumia vocha za elektoniki kutoa msaada wa lishe mjini Harare na Bulawayo. Shirika hilo linakadiria kwamba watu wazima asilia 14.3 ambao ni takribani watu milioni 1.2 wanaishi na virusi vya HIV nchini Zimbabwe na watoto wapatao 150,000 nao wameathirika na kuishi na virusi hivyo.

Katika mpango huu mpya wanaohudhuria vituo vya afya na hospitali na kubainika kuwa na lishe duni wanaelekezwa kwenye vituo vya WFP vya utoaji wa vocha na wanapewa vocha hizo kwa ajili ya kappa chakula kama mafuta ya kupiki na maharage.

Pia wanagawiwa nafaka zenye virtubisho vya hali ya juu ambazo ni mchanganyiko wa mahindi , soya na virutubisho vingine.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud