UM wataka kila mfanyakazi kuhakikishiwa usalama kazini

30 Aprili 2012

Umoja wa Mataifa umesema kuwa usalama wa wafanyikazi ni lazima uwe sehemu ya mabadiliko kwenye uchumi uzioathiri mazingira huku ukionya kuwa iwapo ajira mpya zitachangia katika kutunza mazingira na kubuni nafasi mpya za ajira pia zinaweza kuwa na athari kwa wanaozifanya. Kulingana na shirika la kazi duniani ILO watu milioni mbili wanakufa kila mwaka kutoka na ajali zinazohusiana na kazi huku watu milioni 160 wakiugua magonjwa yanayohusiana na kazi. Mkurugenzi mkuu wa ILO Juan Somavia amesema kuwa mkutano wa kiamataifa wa Rio+20 mwezi Juni unazipa nchi fursa ya kuangali hali ya usalama kazini na usalama kwa ujumla kwenye sayari ya dunia.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud