UNHCR yaanza kuwasambazia wakimbizi wa Afghanistan mahitaji ya kumudu baridi

28 Disemba 2011

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi limeanza kusambaza misaada ya haraka na dharura kwa ajili ya kukabili msimu wa kipindi cha baridi kwa mamia ya wakimbizi walioko huko Afghanistan.

Jumla ya wakimbizi 200,000 wanatazamiwa kupatiwa mahitaji muhimu ambayo yatawawezesha kumudu hali ngumu ya majira ya baridi katika wakati ambapo kunashuhudia kupanda kwa baridi kali katika nchi kadhaa za Asia.

UNHCR ikiwa na washirika wake imekabidhi nguo nzito ikiwemo mablanketi, nguo za kuleta joto pamoja na kusambaza nishati ya mafuta kwa zaidi ya familia 300 na inakusudia kuendelea kutoa huduma hiyo kwa muda wa siku kadhaa

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud