Ban aitilia shime serikali ya Sri Lanka kukamilisha ahadi zake

19 Disemba 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa anamatumaini makubwa kuwa serikali ya Sri Lank itatilia uzito na kutekeleza kwa vitendo ahadi zake ili kulifufua upya taifa hilo ambalo limepitia kwenye vipindi virefu vya vita vya kiraia.

Ban amesema ni matumani yake kwamba serikali itafanya kazi kwa uwazi na ukweli ili kufikia shabaha ya kuliimarisha taifa hilo.

Tayari kamishna ya ukweli na maridhiano imewasilisha ripoti katika bunge la nchi hiyo na Ban amepongeza kutolewa kwa ripoti hiyo akisema kuwa sasa enzi mpya inawadia.

Taifa hilo lililopo barani Asia limeshuhudia vipindi virefu vya machafuko ya kisiasa na kusababisha umwagaji damu mkubwa na kuzorotesha kwa shughuli za kijamii.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud