UNAIDS na benki ya Standard zashirikiana katika kupambana na ugonjwa wa ukimwi

16 Disemba 2011

Shirika la kupambana na ugonjwa wa ukimwi la Umoja la Mataifa UNAIDS limefanya ushirikiano wa miaka miwili na benki ya Standard kwa lengo la kutoa hamasisho kuhusu ugonjwa wa ukimwi barani Afrika.

Kwa kutumia mifumo ya utangazaji wa biashara ya benki ya Standard, UNAIDS itatumia ujuzi wake katika kutoa hamasisho kuhusu ugonjwa wa ukimwi miongonni mwa wafanyikazi wa benki na hadi kwa watu wa kawaida. Benki ya Standard ndiyo taasisi kubwa zaidi ya kifedha barani Afrika na wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani mwaka huu pamoja na washirika wake iliandaa shughuli kwenye mataifa manne yakiwemo Ghana, Nigeria, Uganda na Afrika Kusini. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud