DR Congo na Burundi wajitahidi kupunguza maambukizi ya HIV

16 Disemba 2011

Wakati Ulimwenngu unaadhimisha siku ya kimataifa ya ukimwi, mapema mwezi huu nchi mbalimbali zinajitahidi kukimbizana na wakati ili kuhakikisha moja ya magonjwa sugu yanayoisumbua dunia katika karne hii ya 21, ukimwi, unadhibitiwa na hivyo kukaribia kutimiza lengo namba 6 la milenia ambalo ni kupambana na ukimwi, kifua kikuu na maradhi mengine, ikiwa imesalia miaka mitatu na miezi kadhaa kabla ya kufika mwaka 2015.

Burundi na Jamuhuri ya kidemokasia ya Congo kama baadhi ya nchi zingine za Afrika zimepiga hatua kiasi na zimeanza kushuhudia kupungua kwa maambukizo ya ukimwi.

Kasi ya maambukizi ya Mataifa hayo mawili ya Afrika ya kati imesalia kwenye asilimia nne pekee katika taakwmu za mwaka huu za watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.

Hata hivo kero kubwa bado ni upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya ukimwi ambapo ni idadi ndogo mno ya waathrika wanaonufaika na madawa hayo. Mwandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani Kibuga amefuatilia kwa kina hali halisi baada ya kuzungumza pia na wahusika wakiwemo wagonjwa wa ukimwi na kutuandalia makala hii.

(MAKALA NA RAMADHAN KIBUGA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud