Tanzania imeanza kutoa kipaumbele kwa huduma za ustawi wa jamii lakini bado ni changamoto

25 Novemba 2011

Huduma za ustawi wa jamii ni suala muhimu sana katika maendeleo ya jamii. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa masuala ya familia, watoto, walemavu, wazee na wasio jiweza yasipozingatiwa basi yanaweza kuleta athari kubwa kwa jamii na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Kati nchi zinazoendelea masuala ya ustawi wa jamii bado ni changamoto kubwa kwani kwingine hakuna sera, sheria wala utaratibu wa kuhakikisha huduma hizo zinapewa kipaumbele. Lakini kwa mataifa ambayo yameshaanza kutoa kipaumbele kwa huduma hizo bado wanakabiliwa na shida nyingi ikiwemo fedha.

Leo hii tumetembelewa na Kamishna wa ustawi wa jamii Tanzania Bwana Danford makala na Anna Magige mjumbe kutoka chama cha jumuiya ya wataalamu wa ustwai wa jamii.

Wamekuja Marekani kubadilishana uzoefu kutoko kwa chama cha ustawi wa jamii cha Marekani (National Associationof social workers in the US) ambacho pia kilipeleka ujumbe Tanzania kujifunza hali ya ustawi wa jamii, kuona wanayoyafanya na mapungufu waliyonayo.

Wakizungumza na Flora Nducha wanasema Tanzania bado ina kibarua kigumu kutimiza haja zote za ustawi wa jamii kama anavyofafanua Anna Magige.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud