Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Operesheni za Kenya na serikali ya mpito dhidi ya Al-Shabaab zikikamilika mambo yatakuwa shwari:Mahiga

Operesheni za Kenya na serikali ya mpito dhidi ya Al-Shabaab zikikamilika mambo yatakuwa shwari:Mahiga

Pakua

Mwakilishi maalmu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine Mahiga amesema ana matumaini operesheni za pamoja za kijeshi za serikali ya mpito na Kenya dhidi ya wanamgambo wa Al-Shabaab zikikamilika hali ya amani itakuwa shwari Somalia.

Balozi Mahiga akizungumza na mwandishi wa habari wa radio ya Umoja wa mataifa mjini Nairobi Kenya Jason Nyakundi amesema maeneo yanayoshikiliwa na wanamgambo hao wa kiislamu salama ni mdogo na ni mashirika machache tuu ya misaada ndio yanayoweza kufika. watu wanaendelea kukimbia vita na njaa bado imeshika kasi hasa maeneo ya Kusini mwa Somalia.

Hata hivyo amesema mchakato wa amani unaendelea na sasa ni utekelezaji wa makubaliano yaliyopitishwa hivi karibuni katika mkutano uliofanyika mjini Moghadishu. Sikiliza mahojiano yao.

(MAHOJIANO NA BALOZI MAHIGA)