Kusambaa zaidi kwa ugonjwa wa mafua ya ndege:FAO

29 Agosti 2011

Shirika la kimataifa la chakula na kilimo FAO limetahadharisha juu ya uwezekano wa kusambaa upya kwa ugonjwa wa mafua ya ndege kufuatia ripoti inayoonyesha kuzuka kwa ugonjwa huo katika maeneo ya bara la Asia.

Imeonyesha wasiwasi wake ikisema kazi ya virusi vya ugonjwa huo vinaweza kuvuka mipaka kuanzia bara la asia hadi maeneo mengine na limetaka juhudi za haraka kudhibiti hali hiyo. Tangu kuzuka kwa virusi vya ugonjwa huo yaani H5N1 tayari watu si china ya nane wamefariki dunia huko Cambodia.

FAO imetaka mataifa yote dunia pamoja na washirika wa afya kujiweka katika hali ya utayari ili kukabili virusi hivyo ambavyo vilizuka pia miaka kadhaa iliyopita na kupoteza maisha ya mamia ya wengi.

Virusi vya ugonjwa huo bado vipo katika alama ya juu katika nchi za Bangladesh, China, Misri India, Indonesia na Vietnam. Kumeripotiwa visa vipya vya virusi hivyo katika nchi za Israel na Palestina. Pia hali hiyo inaarifiwa kuwepo nchini Bulgaria, Romania, Nepal na Mongolia.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud