Ukuaji wa miji unashika kasi , ni lazima uende sambamba na miundombinu bora:UN-HABITAT

29 Aprili 2011

 

Mada kuu ya mkutano huo maendeleo endelevu maeneo ya mijini kwa kupitia uwezaji wa kupata ardhi, nyumba, huduma muhimu na miundombinu.

Mawaziri wanaohusika na masuala ya miundombinu na makazi walipata fursa ya kueleza mipango waliyonayo katika nchi zao kuhusu ukuaji wa miji, kuhakikisha unakwenda bega kwa bega na upatikanaji wa huduma muhimu, kulinda mazingira, na maendeleo.

Mwandishi wetu mjini Nairobi Jason Nyakundi alikwenda kwenye mkutano huo na kupata fursa ya kuzungumza na baadhi ya watu waliohudhuria kutoka mataifa ya Afrika na kuandaa makala hii.

(MAKALA NA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud