Mavuno mazuri ya ngano yanatarajiwa Pakistan:FAO

30 Machi 2011

Mavuno yanatarajiwa kuwa mengi kutosheleza kwa chakula watu masikini nusu milioni vijijini. Kwa mujibu wa FAO watu milioni nne watalishwa na chakula hicho katika miezi sita ijayo. FAO imetumia dola milioni 54 za wahisani kwa kununua na kugawa mbegu bora katika mpango maalumu ulioanza Agosti mwaka jana. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)

Mara shughuli za kuvuna zinakapokamilika msaada huo utakuwa umezalisha mazao yenye gharama ya dola milioni 190 ya unga wa ngano ambacho ni chakula kuu kilicho madukani. Mkuu wa huduma za dharura kwenye shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO Daniele Donati anasema kuwa misaada iliyotolewa na wafadhili imeongezeka mara nne zaidi.

Zaidi ya watu milioni 18 waliathiriwa na mafuriko yaliyosababisha uharibifu mkubwa wa nyumba , miundo mbinu pamoja na mimea nchini Pakistan. FAO ilipokea dola milioni 92 kati ya dola 107 ilizoitisha fedha ambazo zimeiwesesha kuinua sekta ya kilimo kwenye mikoa minne iliyoathirika na mafuriko nchini humo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud