Kuundwa serikali mpya Lebanon ni muhimu sana:UM

29 Machi 2011

Serikali ya Lebanon iliyokuwa ikiongozwa na Saad Hariri ilisambaratika Januari mwaka huu baada ya mawaziri 11 wa Izbollah na washirika wao kujiuzulu kwa sababu Rais huyo alikataa kuvunja uhusiano na mahakama inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa inayochunguza mauaji ya baba wa Hariri , ambaye ni Rafik Hariri na wenzie 22 mwaka 2005.

Akitoa taarifa kwenye baraza la usalama la umoja wa Mataifa Bwana Williams amesema amemweleza bayana waziri mkuu wa Lebanon Najib Migati na viongozi wengine kwamba matarajio ya Umoja wa Mataifa serikali mpya itakapoundwa itaendelea kuheshimu majukumu ya kimataifa na hususan azimio namba 1701 la baraza la usalama ambalo nia yake ilikuwa kumaliza vita baina ya Israel na Hizbollah.

Amesema usitishaji mapigano unaendelea kuheshimiwa kwenye eneo la msitari wa Bluu baina ya pande hizo mbili na anatumaini itasalia kubaki hivyo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud