Watoto milioni 28 wadhulumiwa na migogoro:UNESCO

1 Machi 2011

Ripoti hiyo iitwayo mgogoro uliojificha, vita vya silaha na elimu imetahadharisha kwamba dunia haiku katika njia muafaka ya kutimiza lengo namba sita la milenia ambalo linasema elimu wote ifikapo mwaka 2015 lililopitishwa na nchi zaidi ya 60 mwaka 2000.

Ripoti inasema ingawa kuna hatua zilizopigwa lakini nchi nyingi zitashindwa kutimiza lengo hilo hasa zilizo katika vita. Mkurugenzi mkuu wa UNESCO Irina Bokova amesema vita vinasalia kuwa kikwazo kikubwa katika maendeleo ya mwanadamu kwenye sehemu nyingi duniani na athari zake katika elimu zimekuwa zikipuuzwa.

Ripoti hii inabainisha athari zilizojificha za vita katika elimu, chanzo chake na mapendekezo ya kusaidia kuleta mabadiliko.  Ripoti imeongeza kuwa katika jumla ya idadi ya watoto wote wenye umri wa kwenda shule ya msingi duniani kote ambao hawajaandikishwa shule asilimia 42 ambao ni sawa na watoto milioni 28 wanaishi katika nchi masikini zilizoathirika na vita.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo nchi 35 ziliathirika na vita kati ya mwaka 1999 hadi 2008. Nchini Afghanistan mashambulizi 613 yaliripotiwa mwaka 2009 wakati Pakistan washichana 95 walijeruhiwa baada ya mashambulizi shuleni nako Yemen shule 220 ziliharibiwa wakati wa mapigano baiana ya serikali na majeshi ya waasi.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud