Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno La Wiki

UN

JIFUNZE KISWAHILI: METHALI - "USISHINDANE NA KARI KARI NI MJA WA MUNGU"

Katika kujifunza kiswahili tutasikia maana ya methali “USISHINDANE NA KARI, KARI NI MJA WA MUNGU”na mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani. Anaanza kwa kusema kari ni neno linalotokana na neno "karima" au "karama", ambalo linamaanisha zawadi au kipawa maalum kutoka kwa mwenyezi Mungu, ama kweli usishindane na mwenzako, tosheka na kari yako maana yote yatoka kwake mwenyezi Mungu!

Audio Duration
1'12"
UN

NENO: "MUKU"

Na sasa ni wakati wa kujifunza Kiswahili, ambapo leo mtaalam wetu  Onni Sigalla Mhariri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania, anatufafanulia maana ya neno "MUKU"

Sauti
1'4"
UN

Methali: Mwanzo kokochi mwisho nazi

Na leo katika kujifunza Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anatufafanulia maana ya methali, "MWANZO KOKOCHI MWISHO NAZI," karibu!

Sauti
2'4"