Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno La Wiki

Neno la Wiki: SAKARANI

Wiki hii tunaangazia neno “Sakarani” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema neno Sakarani ni msamiati ya kawaida na lina maana tatu, la kwanza ni mtu asiye na akili timamu kutokana na ulevi, ya pili ni mtu ambaye amechanganyikiwa, yaani mwenye akili zisizosawa, na maana ya tatu ni mtu aliyetekwa akili zake kiasi kwamba anashindwa kuvumilia kwa sababu ya kupenda, kumaanisha mlevi wa mapenzi.

Neno La Wiki-Kizaazaa/ Tafrani/ Kizungumkuti

Neno la Wiki ambapo hii leo tunaangazia maneno Kizaazaaa, tafrani na kizungumkuti,  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA .

Bwana Nuhu anasema Kizaazaa ni hali ama mazingira na ni lazima kuwepo na shida, Tafrani ni hisia za mtu, hali ambayo sio ya kawaida na kizungumkuti ni neno linalotokana na mzunguko mzunguko wa kimawazo au hisia.

Neno la wiki: Hanikiza

Wiki hii tunaangazia neno "Hanikiza" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema neno hili lina maana sawa na "hinikiza" ambalo hutumika kama kitenzi kielezi kumanisha sambaza kitu kama vile harufu, mafusho, kelele na kufanya kitapakae sehemu yote. Pia neno "hinikiza" lina minyambuo yake kama vile hinikizia, hinikizwa, hinikizana, hinikizika au hinikizisha.

Neno la Wiki- Sifongo

Wiki hii tunaangazia neno “Sifongo” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema kwamba msamiati huu unafahamika kutokana na kuandikwa sana katika vitabu takatifu. Anasema sifongo ni kama kitu yavu yavu kinachosharabu maji na kina uwezo wa kukaa na maji lakini pia kinayaachia yale maji na hutumika sana kwa kuogea na kujisugulia.

Neno la Wiki- Gozigozi

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia matumizi yasiyo sahihi ya neno gozigozi. Mchambuzi wetu  Nuhu Zubeir Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA anasema neno gozigozi linatumiwa likimaanisha upuuzi au mambo ya hovyo. Lakini kimsingi neno gozi linamaanisha ngozi ya mnyama iliyochunwa na kuachwa hadi ikaoza na pia maana yake nyingine inakwenda katika lugha za kitamaduni. Je ni ipi hiyo? msikilize basi maelezo yake.

Neno la wiki- Jabari

Wiki hii tunaangazia neno Jabari na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema neno hili lina maana zaidi ya moja, maana ya kwanza ni mtawala mkuu wa pekee, maana ya pili ni mtu shujaa asiye na woga na maana ya tatu ni jeuri.

Neno la Wiki - Si ndiyo

Katika neno la wiki Februari 3 tunachambua neno si ndiyo, mchambuzi wetu leo ni, Nuhu Zuberi Bakari ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.