Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno La Wiki

Neno la Wiki: Halisi, Uhalisi, Uhalisia

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno "Halisi", “Uhalisi” na "Uhalisia".  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Ungana naye upate matumizi sahihi ya maneno hayo, ambayo hutumiwa ndivyo sivyo…

Sauti
1'11"

Neno la Wiki: Halisi, Uhalisi, Uhalisia

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno “Halisi”, "Uhalisi" na “Uhalisia”.  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Ungana naye upate matumizi sahihi ya maneno hayo, ambayo hutumiwa ndivyo sivyo...

Je wafahamu maana ya neno mzimu?

Wiki hii tunaangazia neno "Mzimu" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema neno “Mzimu” lina maana zaidi ya moja. Maana ya kwanza ni mahali pa kufanyika matambiko ambayo ni chini ya miti mikubwa kama mbuyu au mkuyu au hata kwenye mapango. Maana ya pili ni kivuli cha sura ya mtu ambaye amefariki dunia. Maana ya tatu ni maskani ya watu waliofariki dunia kama vile makaburini ambako watu wanaweza kwenda kufanya mawasiliano na ndugu zao waliofariki dunia.

Neno la wiki: Zuzu na Bwege

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno "Zuzu" na "Bwege".  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Nuhu anasema zuzu ni mtu ambaye hana akili timamu, mtu ambaye akifunzwa hata hafunziki. Zuzu pia unaweza kumwita mjinga, zezeta au mpumbavu. Bwana Bakari akaenda mbali zaidi kuchambua neno bwege akisema halina tofauti sana na zuzu, kwa maana kwamba ni mtu nduguye. Mathalani bwege ni mtu ambaye amekaa kizoleazolea au mbumbumbu.

Mfiwa huambiwa Makiwa na si pole- Sigalla

Wiki hii tunaangazia neno “Makiwa” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema neno Makiwa ni salamu ya heshima na unyenyekevu inayotolewa kwenye nyumba ya wafiwa. Mtu akiambia Makiwa, mfiwa anajibu "Tunayo" kama marehemu hajazikwa au "Yamepita" kama tayari marehemu amezikwa. Hata hivyo mazoea ni neno "Pole" ambalo mchambuzi anasema halifai sana.

Neno la wiki: Msurupwenye

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno “Msurupwenye”.  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Nuhu anasema Msurupwenye au " Overall" ni gauni inayovaliwa kuzuia uchafu unapofanya kazi ngumu kama vile ya matopematope, useremala au ya kiufundi magari.

Neno la wiki: Kichinjamimba

Wiki hii tunaangazia neno "Kichinjamimba" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema Kichinjamimba ni mtoto ambaye amezaliwa mwishoni kabisa katika idadi ya watoto wa mama.

Neno la wiki: Bwela Suti

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno "Bwela Suti".  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Nuhu anasema “Bwela Suti” ni "apron" au vazi analovaa mtu ili kuzuia uchafu wa mafuta ama vitu vyovyote vile kuharibu nguo zake, aghalabu au hususan hutumika jikoni, lakini pia linawezatumika katika mazingira mengine.

Neno la wiki: Harara

Wiki hii tunaangazia neno “Harara” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema neno "Harara" lina maana nyingi, ya kwaza ni jinsi mtu anavyohisi kuwashwawashwa kwnye ngozi ya mwili, pili ni hali ya mtu kuwa na hasira mbaya ya ghafla, tatu ni hali ya mtu kutokwa na vipele kwenye ngozi, na ya nne ni mbambuko wa ngozi aghalabu kwa watoto au wanawake katika sehemu za mapaja kutokana na joto kali.

Neno la wiki: Kishida na Kibiriti Ngoma

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno “Kishida na Kibiriti Ngoma”.  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Nuhu anasema "Kishida" ni gauni kifupi au kirinda nyepesi kinachovaliwa usiku na mwanamke au msichana anapolala au kinachovaliwa ndani ya nguo, Kibiriti Ngoma ni "mini_skirt" au rinda fupi...