Neno la wiki - Bumbuwazi
Katika neno la wiki hii leo tunaangazia neno "Bumbuwazi". Mchambuzi wetu ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA .
Bwana Nuhu anasema unapopigwa na butwaa ama kupatwa na mshangao, hadi ukawa huwezi kuongea hata neno moja basi utakuwa umepigwa na bumbuwazi.