Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno La Wiki

UN News Kiswahili

Neno la Wiki- OPOA

Wiki hii katika Neno la Wiki, mchambuzi wetu kutoka Baraza la Kiswahili Zanzibar nchini Tanzania , BAKIZA kwa Bi. Mwanahija Ali Juma , Katibu mtendaji wa BAKIZA akichambua maana ya neno  “OPOA”. Anasema kuwa opoa ni lazima kitu kiwe kinatolewa kutoka kwenye maji! Fuatana naye.

Sauti
1'5"
UN News Kiswahili

Neno la Wiki: Aghalabu

Katika kujifunza Kiswahili, Mchambuzi Onni Sigalla wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania “BAKITA” anachambua maana na matumizi ya neno “AGHALABU” ambapo anaeleza maana mbili za neno hilo. Tofauti na ile iliyozoeleka kwa matumizi ambapo neno aghalabu hutumiwa kueleza utokeaji wa mara kwa mara wa jambo, mtaalam huyo ameongeza maana nyingine isiyofahamika sana inayohusishwa na kundi la watu katika jamii au jumuiya.

Sauti
1'1"
UN News Kiswahili

NENO LA WIKI: Kijiko cha jikoni, hakiogopi moto

Neno la wiki limejikita katika kuichambua methali isema, 'Kijiko cha jikoni, hakiogopi moto'.  Mwanariwaya na mwanachama wa Chama Cha Kiswahili cha Kitaifa nchini Kenya, CHAKITA Ken Walibora anasema methali hii kimsingi inaeleza dhana ya kuwa ikiwa mtu ana mazoea fulani au kazoea mazingira fulani, hayamtishi, atatekeleza analolitekeleza bila kuogopa.

Sauti
32"
UN News Kiswahili

Neno la Wiki-Matumizi ya neno AFADHALI.

Aida Mutenyo, mwenyekiti wa idara za Kiswahili katika vyuo vikuu Afrika Mashariki anachambua matumizi ya neno TAFADHALI.  Anasema kuwa nchini Uganda neno hili ni moja ya maneno yanayowasumbua wazungumzaji wa kiswahili kwani wanalichanganya na neno AFADHALI.

Sauti
1'48"