Hatua zachukuliwa kudhibiti athari za COVID-19 kwa wanawake, Uganda
Mlipuko wa COVID-19 tangu ulipoanza umesambaratisha matumaini ya wengi kiuchumi na kijamii kutokana na vikwazo vya usafiri na biashara nyingi zikipigwa marufuku kama njia ya kudhibiti mlipuko huo. Wanawake na wasichana wameathirika zaidi kutokana na hali yao ya uhaba wa rasilimali hali ambayo pia imechochochea vurugu za nyumbani na ukatili wa kijinsia kwa mujibu wa ripoti za serikali mbalimbali.