Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

©UNICEF/Bernardino Soares

Kidato, shule ya mtandaoni Kenya, mkombozi wakati wa Covid-19

Kufuatia kuzuka janga na Covid 19 uvumbuzi wa aina mbalimbali umeshuhudiwa sehemu tofauti duniani ili kuwawezesha watu kuendelea na maisha yao ya kila siku. Nchini Kenya mfanyabiashara Sam Gichuru ameanzisha shule ya mtandaoni kwa jina KIDATO ambayo imewasaidia wanafunzi sehemu mbalimbali duniani kuendela na masomo yao wakiwa nyumbani. Mwandishi wa Kenya Jason Nyakundi amezungumza na Divina Ogari, mmoja wa walimu katika shule hiyo kuweza kufahamu zaidi kuhusu shule ya KIDATO.

Sauti
2'44"
© World Bank/Sarah Farhat

Msichana ajifunza kuendesha tingatinga ili aajiriwe katika sekta ya mafuta, Uganda

Umoja wa Mataifa kupitia malengo ya maendeleo endelevu,  unaendelea kuhamasisha usawa wa kijinsia, kazi za staha na pia ukuaji wa uchumi kwa wanajamii wote. Ili kufikia malengo hayo, ni muhimu kila mtu ashiriki kwa namna tofautitofauti kama alivyofanya msichana mmoja nchini Uganda ambaye ameamua kushiriki mafunzo ya kuendesha Tingatinga ili aweze kunufaika na sekta ya mafuta ambayo inaanza kuchipua nchini Uganda. 

Sauti
3'40"
UNnewskiswahili/Patrick Newman

Taka ya plastiki yapata ufumbuzi jijini Hoima, Uganda

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku ya sayari mama dunia ambayo huadhimishwa kila tarehe 22 ya mwezi Aprili, amesema maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika wakati sayari iko katika hali mbaya wakati binadamu wanaendelea kunyanyasa ulimwengu wa asili. Miongoni mwa changamoto za mazingira na kiafya kote duniani zinasababishwa na matumizi ya plastiki.  

Nchini Uganda hasa katika mji wa Hoima kuna nuru ya kudhibiti madhara ya taka ya plastiki licha ya mbinu za kisheria kugonga mwamba tangu 2009.

Sauti
3'45"
Maktaba

Wanawake katika sanaa wanakumbana na changamoto. Vijana wasiendekeze starehe – Mama Kayai

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, linasema sanaa ianawaleta watu karibu. Sanaa kama vile uigizaji, uchoraji, muziki mathalani wa mababu huzungumza mengi juu ya historia ya ustaarabu na uhusiano unaowaunganisha. 

Inawafanya watu wahisi na kuelewa ni nini kinachounganisha ubinadamu katika utofauti wa tamaduni zake na  hivyo kuchangia katika mustakabali wetu mzuri na endelevu.

Sauti
4'9"
UNESCO/Steven Ripley

Mabadiliko ya tabianchi na madhara yake nchini Kenya

Kupunguza gesi chafuzi zinazochangia katika madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi ni moja ya malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs. . Kwa sasa majanga yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa yanashuhudiwa kila uchao sehemu mbali mbali za dunia, ikiwemo mvua nyingi, mafuriko, ukame mbaya ambao mara nyingi huchangia kutokea njaa. Lakini mabadiliko haya yamaethiri kwa njia gani maisha ya kila siku ya watu nchi za Afrika hususan nchini Kenya?.

Sauti
4'33"
UN Women

Tulikuwa tunawapiga wake zetu lakini elimu imetubadilisha - Wanaume Dodoma.

Ripoti ya hivi karibuni ya shirika la afya la Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa kwa ushirikiano na wadau, imeonesha kuwa mwanamke 1 kati ya 3 sawa na wanawake milioni 736 wanakumbwa na unyanyasaji kama vile vipigo na ukatili wa kingono kutoka kwa wapenzi wao au wanaume wasio wapenzi wao na idadi ya matukio imeonekana kuwa ya kiwango cha juu katika muongo uliopita. Kwa hivyo, Umoja wa Mataifa umeendelea kuhamasisha jamii kote ulimwenguni kuondokana na unyanyasaji wa namna hiyo na aina nyingine zozote za unyanyasaji. Katika hali inayoonekana kuunga mkono wito wa Umoja wa Mataifa, nchini Tanzania

Sauti
4'4"
Restless Development Tanzania

Tunaamini maendeleo ya ulimwengu yanaweza kufanikishwa na kusimamiwa na vijana-Farida Makame 

Ulimwengu ukiwa katika muongo wa kuelekea kufikia utimizaji wa malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu SDGs ifikapo mwaka 2030, shirika lisilo la kiserikali nchini Tanzania, Restless Development, lina imani kubwa kwa vijana kuwa wamekuwa na wanaendelea kuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha malengo hayo hivyo uwekezaji mkubwa inabidi uendelee kuelekezwa kwa kundi hili hasa katika kuwajengea uwezo wa uongozi.

Sauti
3'
© Julius Mwelu/ UN-Habitat

Michezo na vipaji vingine, mkombozi wa vijana, Kibera Kenya

Umoja wa Mataifa unaamini kuwa michezo inaweza kusaidia kuchukua jukumu katika kujenga mnepo na katika kupona dhidi ya janga la COVID-19. Vile vile Umoja wa mataifa unaamini kuwa michezo ina mchango mkubwa katika kuleta maendeleo na amani. Nchini Kenya, katika mtaa wa mabanda, Kibera jijini Nairobi, wakfu wa UWEZA unajaribu kuwasaidia vijana kuweza kujitegemea kwa kutumia vipaji vyao. Miongoni mwa vipaji vinavyolengwa ni pamoja na uchezaji wa mpira wa miguu na uchoraji.

Sauti
4'17"