Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UNICEF/Catherine Ntabadde

Nimepumzisha kazi yangu ya uuguzi ili nipiganie haki za wasichana Pokot, Kenya - Everline Prech

Katika baadhi ya jamii barani Afrika bado zipo tamaduni  ambazo kwa kiasi kikubwa zinawakandamiza wasichana na pia wanawake ingawa ipo mikakati mingi ya kupambana na tamaduni hizo na matunda yanaanza kuonekana. Mwandishi wetu wa Kenya, Jason Nyakundi amemhoji  Everline Prech, mwanaharakati anayepiga vita tamaduni  potovu zinazowakandamiza wasichana na wanawake katika jamii ya Pokot nchini Kenya, jambo ambalo likifanikiwa litakuwa limetoa mchango katika kufikia malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs kufikia kilele chake mwaka 2030.

 

 

Sauti
3'27"
UN Photo/Logan Abassi

Kijana msomi ageukia ufugaji wa nzi ili kunusuru wafugaji wa samaki 

Vijana katika sehemu mbalimbali duniani wameitikia wito wa Umoja wa Mataifa wa kubonga bongo na kusongesha maendeleo yao pale walipo kwa kubaini suluhisho la changamoto zinazokabili jamii inayowazunguka. Miongoni mwao ni Dayana Olembe kutoka Tanzania ambaye baada ya kubaini kuwa wafugaji wa kuku na samaki wanapata shida kupata protini ya kile wanachofuga, akaamua kuingia katika biashara ya ufugaji wa nzi. Ni kweli utashangaa nzi? Ndio!

Sauti
4'36"
UN Women/Ploy Phutpheng

Ufadhili wa Benki ya Dunia, wawasaidia kiuchumi wananchi wa Thailand dhidi ya athari za Covid-19

Kutokana na kuyumba kwa uchumi nchini Thailand kulikosababishwa na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 na kuathiri ajira, kipato na hivyo kuongeza umaskini, hatua za haraka za serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia zimesaidia wananchi kutoangukia katika ufukara. Hali ilikuwa mbaya kiasi kufikia robo ya kwanza ya mwaka 2021 kulikuwa na upungufu wa kazi 710,000 kuliko ilivyokuwa katika robo ya nne ya mwaka 2020. Kiasi cha ufadhili kilichotolewa, asilimia 70 ilipelekwa katika kaya zenye uhitaji zaidi na kiasi kidogo kilichosalia kikaelekezwa katika sekta binafsi.

Sauti
3'10"
UNDP/Sawiche Wamunza

Changamkieni kilimo cha maharage machanga kuinua kipato na kuondoa umaskini- Hadija

Vijana wameitikia wito wa  Umoja wa Mataifa wa kuchukua dhima ongozi katika kufanyia marekebisho na hatimaye kuboresha mifumo ya uzalishaji wa vyakula. Hii ni kuanzia shambani hadi mezani ili hatimaye ifikapo mwaka 2030 suala la ukosefu wa chakula au njaa lisalie kuwa historia sambamba na mifuko ya watu iwe imetunishwa kupitia kilimo bora na cha kisasa, na hivyo kufanikisha lengo la kwanza la malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs, la kutokomeza umaskini.

Sauti
4'24"
© IOM 2021/Lauriane Wolfe

Bia aliyonyweshwa msichana mwingine yageuka mahari ya mtoto na kisha akabakwa!!!

Siku ya kimataifa ya kukabiliana na usafirishaji haramu wa kibinadamu huadhimishwa kila tarehe 30 ya mwezi Julai. Mwaka huu ujumbe ni Manusura wa  usafirishaji haramu binadamu wawe msingi wa kampeni dhidi ya vitendo hivyo. Hii ni kwa kuzingatia kuwa mara nyingi manusura hupuuzwa,  watu wanashindwa kuwaelewa na hata kile walichopitia huwa hakipatiwi kipaumbele kama njia ya kujifunza, kurekebisha na kuokoa wengine walionasa kwenye mtego huo.

Sauti
3'7"
UN/ John Kibego

Covid-19 imeathiri kazi yangu ya ualimu na sasa ninauza juisi – Mwalimu Catherine Tuhaise 

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na kutangazwa na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa ILO, tayari umeweka wazi kuwa kumekuwa na upotevu mkubwa wa ajira duniani. Na utafiti unaenda mbali zaidi kwamba wanawake wataathirika zaidi katika siku zijazo. Hali halisi tayari inaonekana katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu ambako hatua kadhaa zilizochukuliwa ili kuudhibiti ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona, zimesababisha watu kupoteza vyanzo vyao vya mapato.

Sauti
3'44"