Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

© UNFPA Myanmar/Yenny Gamming

Wazazi tulinde watoto wetu dhidi ya mimba katika umri mdogo - Catherine Kobusinge Kamanyire

Nchini Uganda ripoti kutoka wilaya mbalimbali zinaonesha ongezeko la idadi ya wasichana waopata mimba utotoni kuliko wakati wowote kabla ya shule kufungwa kutokana na COVID-19. Wakati wilaya ya Hoima pekee imeripoti mimba za utotoni zaidi ya 6,000 wilaya jirani ya Masindi imeripoti zaidi ya wasichana 1,500 waliopata mimba kati ya mwezi Januari na Juni mwaka huu.

Uganda ina takribani wilaya 135.

Sauti
3'53"
Stephan Gladieu/World Bank

Mradi wa Benki ya Dunia waleta tumaini kufikia ajenda 30, Uganda

Mradi wa kuhakikisha maendeleo endelevu katika eneo lenye rasilimali ya mafuta nchini Uganda umeleta matumaini ya kukabili umaskini baada ya masoko kujengwa na barabara kadhaa katika wilaya tatu za eneo hilo.Je, mradi huo wa ARSDP unaofadhiliwa na Benki ya Dunia unasaidiaje? Basi ungana na mwandishi wetu wa Uganda John Kibego ambaye emezungumuza na viongozi wa mitaani kwenye ziara ya ukaguzi ya waziri wa maendeleo ya miji. 

Sauti
3'26"
UN News/ John Kibego

"Ningekuwa mbali katika muziki isingekuwa vita" – Mkimbizi nchini Uganda

Katika kuchagiza amani na upendo miongoni mwa wakimbizi, kijana Fideli Karafuru Busimba mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, anatumia kipaji chake cha usanii kusambaza ujumbe wa upendo na amani hasa wakati huu wa changamoto zinazotokana na mlipuko wa COVID-19 akiwa ukimbizini nchini Uganda. Kijana huyu ambaye pia ana ujuzi wa uchoraji na useremala, anaomba kupatiwa hifadhi katika nchi ya pili ukimbizini akiamini kuwa itamsaidia kuepuka changamoto za kifedha zinazokwamisha ndoto zake katika maisha.

Sauti
3'42"
UNICEF

Wanafunzi wenye ualbino waona nuru, ni matunda ya azimio la Durban

Tarehe 22 mwezi huu wa Septemba viongozi wa nchi na serikali wanaohudhuria mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa watashiriki mkutano wa ngazi ya juu wakimulika miaka 20 tangu kupitishwa kwa azimio la Durban la kupinga aina zote za ubaguzi ikiwemo rangi na makundi mbalimbali kama vile watu wenye ualbino. Nchini Tanzania hatua zimechukuliwa na sasa kuna mazingira rafiki kwa watu hao kama anavyosimulia Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC, nchini humo alipotembelea mkoani Mwanza.

Sauti
4'1"
UN News/ John Kibego

Tafuteni fursa badala ya kuangalia tu madhara ya COVID-19 – Mzee nchini Uganda

Je, wafahamu kwamba kuna fursa kati ya changamoto zilizosababishwa na mlipuko wa covid-19 duniani? Wakati baadhi ya watu wamevunjika moyo baada uchumi kudorora huku wengine wakikabiliwa na changamoto za malazi na upatikanaji wa chakula katika maeneo ya mijini, bado kuna matumaini ya kufanya makubwa zaidi ikiwemo uvumbuzi utakaosaidia hata baada ya corona.

Sauti
3'33"