Zama za kale si kama za sasa mtoto Angela abaini kutoka kwa nyanya yake Muthoni:UNICEF
Kutana na Angela Andia mshindi wa mwaka 2021 wa mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF uitwao “wisdom project” au mradi wa busara ambao unashirikisha watoto wa umri wa kati ya miaka 9-14 kila mwaka wakishindana katika kuandaa Habari zinazohusu haki za mtoto nchini Kenya.