Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Rais Nkurunziza akatisha safari kwenye UM baada ya mauaji nchini Burundi

Watu wasiopungua 40 wameuwawa nchini Burundi katika shambulio la watu wenye silaha kwenye wilaya ya Gatumba nje kidogo ya mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura . Serikali ya Burundi imetangaza msiba wa kitaifa na maombolezo kwa siku tatu.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ambaye angeianza ziara hii leo kuelekea nchini Marekani kuhudhuria kikao cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa ambalo limeanza kujadili maradhi yasiyo ya kuambukiza ameahirisha safari yake.

Mwandishi wetu wa Burundi Ramadhan Kibuga na taarifa kamili.

(RIPOTI YA RAMADHAN KIBUGA)

Bila kujua kusoma na kuandika hakuna maendeleo:UM

Wiki hii dunia imeadhimisha siku ya kimataifa ya kujua kusoma na kuandika, takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa watu zaidi ya milioni 700 duniani na hasa watu wazima hawajui kusoma na kuandika.

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO limesema bila kufuta ujinga kwa kujua kusoma na kuandika ambayo ni haki ya binadamu, basi maendeleo yatasalia kuwa ndoto katika jamii nyingi.

Bila kujua kusoma na kuandika kuendelea ni vigumu:M

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya kufuta ujinga kwa kujua kusoma na kuandika, Umoja wa Mataifa unasema bila kutatua tatizo hilo linalowakabili watu zaidi ya milioni saba duniani amani na maendeleo itaendelea kuwa ndogo.

Pamoja na juhudi kubwa zinazoendelea lakini bado wanawake wengi na wasichana hawajapata fursa ya kujua kusoma na kuandika hasa kwenye nchi zinazoendelea na hususani maeneo ya vijijini, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiungwa mkono na mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO.

Mkutano wa kuomba msaada kwa ajili ya pembe ya Afrika kufanyika Addis Ababa

Mkutano wa Kimataifa ulioandaliwa na Umoja wa Afrika kwa ajili ya kuomba msaada wa kukabiliana na matatizo yanayoikabili pembe ya Afrika hivi sasa utafanyika kesho Alhamisi mjini Addis Ababa Ethiopia.

Lengo la mkutano huo ni kuonyesha mshikamano kwa waathirika wa ukame na njaa kwenye pembe ya Afrika, na Umoja wa Afrika umeziomba nchi wanachama kukusanya fedha zitakazosaidia kuokoa maisha ya mamilioni ya watu wanaohitaji msaada wa dharura hivi sasa hususani Somalia, Ethiopia, Djibouti na Kenya.

Burundi kuongoza wanajeshi kulinda amani Somalia

Rais wa Burundi Pierre Nkrunziza amesema nchi yake itaongeza idadi ya vikosi vyake vinavyolinda amani nchini Somalia chini ya mwamvuli wa vikosi vya Umoja wa Afrika AMISOM.

Tamko la Rais Nkurunziza limekja baada ya ziara ya Rais Sheikh Shariff Sheikh ahmed wa Somalia mjini Bujumbura na kutanabaisha umuhimu wa vikosi hivyo vya kulinda amani kongezwa.

Nchi za pembe ya Afrika zaendelea kukumbwa na uhaba mkubwa wa chakula

Ripoti zimekuwa zikitolewa kuhusu hali kwenye pembe ya Afrika baada ya eneo hilo kukumbwa na ukame wa muda mrefu. Kwa sasa kuna uhaba mkubwa wa chakula nchini Somalia , Ethiopia , Kenya na Uganda hali ambayo huenda ikawa janga kubwa zaidi dunia ikiwa hatua za dharura hazitachukuliwa kulingana na mkuu wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Antonio Gutteres . Msemaji wa UNHCR nchini Kenya Immanuuel Nyabera amezungumza na mwandishi wetu Jason Nyakundi na kumwelezea jinsi hali ilivyo.

(MAHOJIANO YA JASON NA IMMANUEL NYABERA )

Dr wa Hospitali ya Panzi DR Congo ataka ushirikiano zaidi na UM

Dr Denis Mukwege, mkuu wa hospitali ya Panzi mjini Bukavu iliyoko Kivu ya Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na kumuelezea nia ya ushirikiano baina ya hospitali yake, Umoja wa mataifa na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Congo MONUSCO kwa ajili ya kunsuru maisha ya maelfu ya wanawake wanaobakwa nchini Congo.

Dr wa hospitali inayoungwa mkono na UM DR Congo apata tuzo

Dr Denis Mukwege, mkuu wa hospitali ya Panzi mjini Bukavu iliyoko Kivu ya Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ametunukiwa tuzo ya kiamataifa na ufalme wa Ubelgiji mwezi Mai mwaka huu kwa mchango wake katika jamii.

Tuzo hiyo ya kimataifa ambayo hutolewa kila baada ya miaka miwili humuendea mtu ambaye amechangia kwa kila hali kuendeleza maendeleo duniani.

MKURABITA yaitwalia Tanzania tuzo ya UM ya utumishi wa umma

Mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania MKURABITA umeisaidia Tanzania kujinyakulia tuzo ya utumishi wa umma Tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwaka na Umoja wa Mataifa hasa kwa kuangalia ubunifu wa kuweza kuharakisha huduma nzuri kwa umma.

Baada ya kushika nafasi ya pili mwaka jana mwaka huu Tanzania imeshika nafasi ya kwanza barani Afrika. Tuzo hiyo imetolewa sambamba na kongamano la kimataifa la utumishi wa umma linalofanyika jijini Dar es salaam Tanzania kuanzia Juni 20 na litakamilika june 23.