Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

29 JANUARI 2024

Hii leo kwenye Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa Anold Kayanda anaanzia na masuala ya afya, hususan viambato vya mafuta vinavyohatarisha afya ya mwili, kisha miradi ya UN ilivyosaidia wanawake huko Syria .Makala inakupeleka Angola kuona jinsi Umoja wa Mataifa umenusuru wanawake wa vijijini kwa hohehahe na mashinani atakupeleka katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko Kaunti ya Turkana, nchini Kenya kupata ujumbe kuhusu elimu hasa kwa wasichana.

Sauti
11'44"
UNICEF TANZANIA

Hata mimi mwenyewe nilikuwa sijiamini hadi nilipopata mafunzo ya RLabs - Mariam

Mkakati wa Afya ya Uzazi kwa Wasichana, Haki, na Uwezeshaji nchini Tanzania (GRREAT) unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na wadau likiwemo shirika lisilo la kiserikali la RLabs Tanzania na serikali ya Canada ni mpango wa miaka mitano (2019-2024) ili kuisaidia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuboresha ustawi wa wasichana balehe katika mikoa ya Mbeya na Songwe, pamoja na Zanzibar.

Sauti
3'14"