Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

26 JULAI 2022

Hii leo jaridani Anold Kayanda anakuletea Habari kwa Ufupi; Mada Kwa Kina na Mashiani:

Katika Mada kwa Kina anasalia makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambako wiki iliyopita Naibu Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Amina J, Mohammed alizindua maonesho ya “Ulikuwa umevaa nini? Yakionesha nguo ambazo walivalia manusura wa ukatili wa kingono, kwa kuzingatia kuwa jamii humbebesha lawama ya kubakwa yule aliyebakwa badala ya aliyebakwa kwa kisingizio cha mavazi.

Sauti
12'24"

25 JULAI 2022

Hii leo jaridani tunaanza na siku ya kimataifa ya watu kuzama majini na Umoja wa Mataifa unataka hatua zaidi kuepusha watu kuzama majini kutokana na hali hiyo kuwa sababu inayoongoza kwa vifo vitokanavyo na ajali. Kisha tunabisha hodi Kenya ambako UNICEF inatoa wito kwa serikali itakayoingia madarakani kwenye uchaguzi mkuu ujao ipatie kipaumbele hifadhi ya jamii. Makala tunakwenda DRC kuona jinsi walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanatoa misaada kwa wanafunzi ili wajifunze Kiswahili na hatimaye wachangie katika kusongesha amani.

Sauti
11'33"

22 JULAI 2022

Hii leo jaridani kubwa ni kutiwa saini huko Istanbul Uturuki kwa makubaliano baina ya Urusi, Ukraine na Umoja wa Mataifa ya kuwezesha nafaka na vyakula kutoka Ukraine viweze kusafirishwa kupitia Bahari Nyeusi. Shuhuda wa Umoja wa Mataifa kwenye utiaji huo saini si mwingine bali ni Katibu Mkuu mwenyewe wa UN, Antonio Guterres.

Sauti
12'59"

21 JULAI 2022

Hii leo jaridani ni siku ya mada kwa kina, halikadhalika kuna Habari kwa Ufupi bila kusahau kujifunza lugha ya Kiswahili. Mada kwa kina inakupeleka Kaunti ya Migori nchini Kenya kumulika harakati za Umoja wa Mataifa kusaidia wakulima kuondokana na kilimo hatarishi cha tumbaku.

Sauti
10'46"

20 JULAI 2022

Hii leo katika jarida tunamulika doria zinazoendeshwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Sudan Kusini, UNMISS jimboni Tambura, kisha sakata la kupungua kwa ukubwa wa chapati huko kambini Dzaleka nchini Malawi kutokana na COVID-19 na vita ya Ukraine kwa kuwa gharama za bidhaa zimeongezeka.

Sauti
12'53"

19 JULAI 2022

Hii leo jaridani tuna mada kwa kina mahsusi ikimulika raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC aitwaye Esperance Tabisha aliyenufaika na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuhamishia wakimbizi nchi ya tatu kupitia mkataba wa kimataifa wa wakmbizi, GCR. Katoka DRC kaingia kambini Kakuma nchini Kenya na kisha Canada na sasa ni mbunifu wa mitindo akitumia mtandao wa kijamii kupata wateja wake. Janga la COVID-19 lilikuwa chungu na tamu hapo hapo kwa vipi? Thelma anasimulia.

Sauti
12'5"

18 JULAI 2022

Hii leo jaridani tunamulika siku ya kimataifa ya Nelson Mandela kwa kukutelea ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuhusu nafasi ya hayati Mandela katika maendeleo na amani. Tunaangazia pia tamko la mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Haki ya Afrika wa kuamuru Kenya ilipe fidia jamii ya asili ya Ogiek kwenye msitu wa Mau. Makala ni mchezo wa kuigiza wa kushawishi wajawazito kwenda kliniki wakiwa na waume zao na Leah Mushi anakupeleka nchini Malawi.

Sauti
9'48"

15 JULAI 2022

Hii leo jaridani kubwa kabisa ni siku ya kimataifa ya stadi kwa vijana ambapo tunaanza kwa kupata ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akisisitiza marekebisho ya mafunzo ya stadi kwa vijana na kisha tunapata mfano kutoka mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania ambako huko tayari UNDP imepatia vijana mafunzo stadi ya kilimo  bora na ufugaji. 

Sauti
11'34"

14 JULAI 2022

Jarida la leo lina Habari kwa Ufupi, Mada kwa Kina na Jifunze Kiswahili.

Katika Habari kwa Ufupi, Leah Mushi anamulika wito wa UNHCR wa kutaka sitisho la mapigano huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako watu wanauawa na maelfu wanafurushwa. Kisha anamulika ripoti ya Umoja wa Mataifa kuwa ujira wa wanawake kwenye sekta ya afya ni wa chini kulinganisha na wanaume hata kama wako katika ngazi moja na mwisho ni wito kutoka UNCTAD wa kutaka bara la Afrika lisitegemee tu mazao na madini kupata fedha za kigeni bali iuze bidhaa za kihuduma.

Sauti
12'15"

13 JULAI 2022

Hii leo katika jarida tunamulika utafiti ambao WHO inafanya ili kubaini aina mpya ya ugonjwa wa homa ya ini kali au Hepatitis B ambayo inakumba watoto, ugonjwa umepatikana kanda zote za WHO isipokuwa Afrika. Kisha tunakwenda Haiti kuangazia changamoto za kiuchumi, kijamii na kiusalama lakini Umoja wa Mataifa haukati tamaa unaendelea kupeleka misaada ya kibinadamu .Makala inammulika Priscilla Lecomte, raia huyu wa Ufaransa ambaye anazungumza lugha ya Kiswahili kwa ufasaha na sasa naona nafasi kubwa ya lugha hiyo katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Sauti
10'13"