Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

12 SEPTEMBA 2022

Hii leo jaridani Flora Nducha anaanza kwa taarifa ya kwamba utumwa wa kisasa una aina mbalimbali ikiwemo kwenye ajira na pia kwenye ndoa. Kisha anakupeleka kaunti ya Tukrana nchini Kenya ambako UNICEF imenusuru wanawake na mwendo mrefu wa kusaka maji kwa kuwajengea mabwawa ya mchanga. Makala anakukutanisha na Hamad Rashid wa redio washirika MVIWATA FM mkoani Morogoro akikuletea mradi wa UNCDF ambao umekwamua maisha ya wakazi wa Kibondo mkoani Kigoma Tanzania kupitia ushirika wa kilimo uitwao Kibondo Big Power Group.

Sauti
11'48"

09 SEPTEMBA 2022

Katika Jarida la habari la Umoja wa Mataifa leo Ijumaa Flora Nducha anakuletea

-Katika siku ya kimataifa ya kulinda shule dhidi ya mashambulizi mashirika ya Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na la elimu sayansi na utamaduni UNESCO yanasema Afrika ya Kati na Magharibi ni nyumbani kwa karibu robo ya watoto wote duniani wasiokwenda shule  

Sauti
10'59"

08 SEPTEMBA 2022

Katika jarida la mada kwa kina hii leo kutoka Umoja wa Mataifa, Flora Nducha anakuletea 

-Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Maendeleo UNDP kuhusu maendeleo ya binadamu inaonyesha kuwa maendeleo hayo ya binadamu ynashuka kwa karibu asilimia 90 ya nchi duniani

Sauti
13'15"

07 SEPTEMBA 2022

Katika jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea 

-Katibu Mkuu UN atoa wito kwa ushirikiano wa kimataifa kukabiliana na uchafuzi wa hali ya hewa katika siku ya kimataifa ya hewa safi kwa ajili ya anga ya bluu

-Hatuwezi kusubiri hadi baa la njaa litangazwe Somalia tunafanya kila tuwezalo kuwanusuru Wasomali limesema shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP 

Sauti
12'18"

06 SEPTEMBA 2022

Katika Jarida la mada kwa kina hii leo Flora Nducha anakuletea

-Mashirika ya misaada ya kibinadamu yamesema Somalia imefikia kkatika hali mbayá sana. Maisha ya mamia ya maelfu ya watu yamo hatarini hivi sasa kutokana na tathimini iliyofanywa hivi karibuni kuhusu uhakika wa chakula na lishe. Baa la njaa linajitokeza katika wilaya za Baidoa na Burkhakaba kwenye jimbo la Bay lina uwezekano wa kudumu hadi Machi 2023 ikiwa msaada wa kibinadamu hautaongezwa kwa kiasi kikubwa na mara moja.

Sauti
11'51"

02 Septemba 2022

Ungana na Flora Nducha anayekuletea jarida kutoka kila kona ya dunia na kuanzia huko Pakistan

- Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanafanya kila juhudi kuhakikisha yanasaidia zaidi ya watu milioni 33 walioathirika na mafuriko nchini Pakistan baada ya mvua za monsoon kunyesha kwa kiwango kikubwa sana na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1200 huku yakiharibu kabisa miundo mbinu mingine. 

Sauti
12'23"

01 SEPTEMBA 2022

Katika Jarida la mada kwa kina hii leo Flora Nducha anakuletea

-Msimu mpya wa shule ukianza sehemu mbalimbali duniani , takwimu mpya zilizotolewa leo mjini Paris Ufaransa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO zinaonyesha kwamba watoto na vijana milioni 244 wenye umri wa kati ya miaka 6 na 18 duniani kote bado hawako shule.

-Mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths leo ameanza ziara nchini Somalia kushuhudia hali halisi ya njaa na kutathimini mahitaji ya walioathirika na ukame na hatua zinazochukuliwa kuwasaidia.

31 AGOSTI 2022

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea 

-Leo ni siku ya kimataifa ya watu wenye asili ya Afrika, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anasema licha ya mchango wao mkubwa bado wanaendfelea kubaguliwa kote duniani.

-Meli iliyosheheni msaada wa chakula kilichonunuliwa na shirika la mpango wa chakula duniani WFP kutoka nchini Ukraine kwenda Ethiopia imetia nanga jana nchini Djibout tayari kusambazwa kwa msaada huo

Sauti
10'50"

30 AGOSTI 2022

Katika jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea 

-Nusu ya vituo vya huduma za afya duniani kote vinakosa huduma za usafi na hivyo kuwaweka wagonjwa na wahudumu wa afya katika hatari kubwa ya kusambaza magonjwa na maambukizi kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na WHO na UNICEF.

Sauti
12'56"

29 AGOSTI 2022

Flora Nducha anakuletea jarida lililo sheheni habari mbalimbali kuanzia nchini Ethiopia ambapo tume ya Kimataifa ya wataalamu wa Haki za binadamu nchini Ethiopia imekasirishwa na kuzuka upya kwa uhasama kati ya serikali ya Ethiopia na chama cha Tigray People's Liberation Front tangu wiki iliyopita na kuzitaka pande zote mbili kurudi kwenye meza ya mazungumzo kwani wanaoteseka ni raia.

Wakimbizi wa Burundi wakioko katika kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma nchini Tanzania wameshukuru kwa watoto wao kupatiwa vyeti vya kuzaliwa 

Sauti
10'26"