Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

07 DESEMBA 2022

Hii leo jaridani tuanamulika Upper Nile nchini Sudan Kusini na nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala tunakwenda nchini Kenya na mashinani tunakuletea ujumbe. Kuhusu ukatili wa kijinsia.

Sauti
12'53"

06 DESEMBA 2022

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na tukiwa tungali katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana duniani, tunamulika wale wanaowapokea manusura wa ukatili wa kijinsia nchini Kenya. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani kutoka Uganda.

Sauti
12'13"

02 DESEMBA 2022

Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya WHO, habari kutoka Rwanda, makala inayomulika harakati za Umoja wa Mataifa za kusaidia wakulima wenye ulemavu na mashinani tunakwenda nchini Burkina Faso.

Sauti
11'42"

1 DESEMBA 2022

Leo ni Siku ya Ukimwi duniani na jarida linakuletea mada kwa kina tukijikita kabisa nchini Nigeria, moja ya nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ambako ripoti inasema hali si shwari ya maambukizi.  Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani  

Sauti
13'4"

30 NOVEMBA 2022

Jaridani leo tunaangazia mtandao wa intaneti barani Africa na juhudi za UNICEF Uganda katika shule moja ya msingi nchini humo. Makala tutaelekea nchini Tanzania Kusini Magharibi katika mkoa wa Mbeya na mashinani tutasalia hukohuko nchini Tanzania katika kambi ya wakambizi ya Nyarugusu.

Sauti
12'18"

29 NOVEMBA 2022

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina tukiangazia juhudi za kuwajengea watoto tabia ya kupenda kusoma vitabu na pia habari kwa ufupi zikiwemo ripoti ya UNAIDS na WHO, na usaidizi kwa wakimbizi na jamii za wenyeji nchini Chad. Mashinani tutakwenda nchini Cameroon, kulikoni?

Sauti
13'47"

28 NOVEMBA 2022

Hii leo jarida linakuletea habari za WHO na michuano ya fainali za Kombe la Dunia. Makala inatupeleka kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya kusikia simulizi ya msichana mnufaika wa mradi wa Girl Shine na Mashinani tutaelekea nchini Uganda kwa mkimbizi mwanaharakati wa mazingira

Sauti
10'56"

25 NOVENBA 2022

Hii leo jarida linaangazia afya nchini Haiti na ujenzi wa amani hasa kwa lengo la kuepusha vijana kutumbukizwa kwenye vikundi vyenye msimamo mkali huko Garissa nchini Kenya. Makala tunakwenda nchini Poland na Mashinani nchini Ethiopia, kuliko ni?  

Sauti
10'28"

23 NOVEMBA 2022

Hii leo jarida linamulika ukatili dhidi ya wanawake na wasichana na pia mradi wa kupatia fedha jamii nchini Malawi. Makala tunakwenda nchini Kenya na Mashinani nchini Tanzania.

Sauti
14'25"