Jarida la Habari

Hatari ya viuavijidudu kwenye mbogamboga yamulikwa Uganda 

Ni wazi kuwa mbogamboga ni muhimu katika kuongeza damu na kinga dhidi ya magonjwa mwilini, lakini Je, wafahamu kwamba mbinu za kisasa za kilimo zaweza kugeuza virutubisho kuwa sumu? Na je, unajua kwamba unaweza kutumbukia kwenye magonjwa hatari na kupoteza maisha usipokuwa makini?

Sauti -
3'22"

25 Februari 2021

Jaridani hii leo Flora Nducha anamulika teknolojia na hatua ambazo serikali zinapaswa kuchukuliwa ili ziweze kunufaisha kila mtu na zilete maendeleo ya watu. Watunga sera wakiwemo wabunge wana jukumu lao, ni kutoka UNCTAD.

Sauti -

24 Februari 2021

Hii leo jaridani tunaanzia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako wananchi licha ya madhilla wanayopitia mashariki mwa nchi hiyo wanashikamana na wanasaidiana ili angalau kupunguza machungu.

Sauti -

23 Februari 2021

Hii leo jaridani Flora Nducha anaanzia na ripoti mpya ya shirika la kazi la Umoja wa Mataifa, ILO ikiangazia majukwaa mapya ya ajira dunia

Sauti -

22 Februari 2021

U hali gani siku ya leo Jumatatu Februari 22 mwaka 2021 na mwenyeji wako Flora Nducha anakueletea mada kwa kina akimulika lugha ya mama, kwa kuzingatia kuwa tarehe 21 mwezi Februari ni siku ya lugha ya mama duniani.

Sauti -
11'7"

19 Februari 2021

Leo ni Ijumaa na kama ilivyo ada ni mada kwa kina na tunakwenda Darfur nchini Sudan hususan eneo la Khor Abeche ambako hatimaye wiki hii kambi ya Khor Abeche iliyokuwa inatumiwa na walinda amani wa Tanzania katika UNAMID imekabidhiwa rasmi kwa serikali ya Sudan kufuatia kukamilika kwa majukumu ya

Sauti -
12'41"

18 Februari 2021

Hii leo jaridani Flora Nducha anaanza na masuala ya mazingira ambapo ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inasema bado safari ni ndefu kukabili mabadiliko ya tabianchi. Kisha anabisha hodi Msumbiji ambako anaangazia msaada kwa manusura wa dhoruba kali Eloise.

Sauti -

17 Februari 2021

Hii leo jaridani Flora Nducha anaanzia nchini India ambako mwalimu mmoja wa kiume ameshinda tuzo ya Mwalimu Bora Duniani kwa mwaka 2021 kwa mchango wake katika kutumia uwezo wake kuboresha elimu bila kujali kipato chake.

Sauti -
12'10"

16 Februari 2021

Hii leo jaridani Flora Nducha aanza na ombi la dola milioni 222 kwa ajili ya wakimbizi wa Burundi waliosaka hifadhi nchi jirani za Tanzania, DRC na Rwanda.

Sauti -
13'12"

15 Februari 2021

Hii leo jaridani siku ya Jumatatu ni mada kwa kina na tunamulika nafasi ya redio katika jamii ya sasa na jinsi watangazaji walivyokwenda na wakati ili kuhakikisha chombo hicho adhimu kinaendelea kutekeleza majukumu yake.

Sauti -
10'52"