Jarida la Habari

28 Juni 2019

Ijumaa kama kawaida tuna muhtasari wa habari na kubwa zaidi ni mauaji ya watu 117 huko Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kufuatia mapigano kati ya kabila la walendu na wahema, mauaji hayo ni kati ya tarehe 10 na 13 mwezi huu wa Juni.

Sauti -
9'57"

26 Juni 2019

Leo siku ya kimataifa ya kupiga vita matumizi na usafirishaji wa madawa ya kulevvya tunaanzia nchini Tanzania ambako vituo vya Back To Life vya kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya vimekuwa msaada mkubwa kwa kundi hilo.

Sauti -
12'33"

25 Juni 2019

Je wafahamu dagaa na samaki wadogo kutoka mtoni na ziwani ni muarobaini wa lishe bora na kutokomeza umaskini? Imesema

Sauti -
12'14"

21 Juni 2019

Hii leo Ijumaa, jarida lina mada kwa kina ikibisha hodi huko nchini Kenya kwa mpishi mkuu Ali Mandhry, al maaruf Chef Ali, akimulika gastronomia, au sayansi ya mapishi! Je wafahamu ni nini?

Sauti -
9'56"

20 Juni 2019

Je wajua kuwa vita na mizozo husababisha kiwewe kwa watoto na kuwafanya washindwe kujifunza hata wakiwa ugenini? Ndio maana leo UNESCO inataka walimu wapatiwe mafunzo ili wahimili changamoto za kufundisha watoto wakimbizi wenye kiwewe. Hii ni moja ya habari zetu leo siku ya wakimbizi duniani.

Sauti -
11'48"

19 Juni 2019

Leo ni siku ya kimataifa ya kukabiliana na ukatili wa kingono kwenye maeneo ya mizozo na tunamulika kauli ya Umoja wa Mataifa inayosema kuwa ukatili huo ni msalaba kwa wote na hivyo hatua zichukuliwe kusaidia manusura.

Sauti -
12'57"

18 Juni 2019

Hii leo tunaanzia Uganda kuangalia mtazamo wa wananchi katika harakati za kukabili Ebola na mwandishi wetu John Kibego amevinjari Buliisa. Huko DRC nako si shwari walendu na wahema wapigana na maelfu wafurushwa.

Sauti -
12'32"

17 Juni 2019

Hii leo jaridani tunaanza na wito kwa kila mkazi wa dunia kuhakikisha anachukua hatua kuepusha kuenea kwa jangwa na mmomonyoko wa ardhi.

Sauti -
12'26"

14 Juni 2019

Hii leo Ijumaa ni mada kwa kina ikimulika mtoto wa kike nchini Tanzania mwenye umri wa miaka 16 ambaye amebuni apu ya kukumbusha wanawake wajawazito kuhusu ujauzito wao na kwenda kliniki.  Ubunifu wenye tija kwenye mazingira yake.

Sauti -
10'33"

13 Juni 2019

Miongoni wa Habari za zinazoletwa kwako na arnold Kayanda katika jarida la leo ni 

-Siku ya kimataifa ya uelimishaji dhidi ya ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi, utamsikia mwanamuziki Lazarus kutoka Malawi mlemavu wa ngozi ambaye sasa maisha yake yamebadilika

Sauti -
11'50"