Jarida la Habari

31 Mei 2019

Katika Jarida kwa Kina hii leo Flora Nducha anaangazia

-Mkutano wa kimataifa wa ufadhili kwa ajili ya Msumbiji baada ya vimbunga Idai na Kenneth

-Serikali ya Tanzania imesema kuanzia kesho Juni Mosi ni marufuku kutumia mifuko ya plastiki

Sauti -
9'57"

30 Mei 2019

Hii leo tunaanzia Ujerumani ambako Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres amepokea tuzo ya mwaka huu ya Charlmangne inayopatiwa watu wanaochangia muungano wa Ulaya, ambapo mwenyewe kasema tuzo hiyo si yake bali ya wanawake na wanaume wa Umoja wa Mataifa wanaochangia kusongesha maadili ya Ulaya ulimwe

Sauti -
11'46"

29 Mei 2019

Ulinzi wa amani si chaguo ni wajibu ambao kila mtu katika jamii anapaswa kuuvaa, asema mrakibu mwandamizi wa polisi Martha Neema Mlay kutoka nchini Tanzania ambaye ni miongoni mwa walinda amani wanawake waliowahi kushiriki kwenye opresheni za Umoja wa Mataifa. Leo ni siku ya walinda amani duniani

Sauti -
12'50"

28 Mei 2019

Jaridani Mei 28, 2019  na Flora Nducha 

Zaidi ya watu 20,000 wafungasha virago Nigeria kukimbia machafuko na kusaka usalama Niger

Baraza la afya duniani lakunja jamvi leo Geneva na kutangaza mikakati maalum.

Sauti -
12'22"

27 Mei 2019

Ikiwa leo ni siku ya mapumziko nchini Marekani ambapo inasherehekewa siku ya kuwakumbuka mashujaa, tunakuletea jarida maalumu kuhusu ugonjwa wa Fistula. Utawasikia wagonjwa na pia madaktari. Elimika.

Sauti -
9'53"

24 Mei 2019

Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kumefanyika maadhimisho ya siku ya walinda amani duniani ikienda sambamba na utoaji wa nishani kwa walinda amani waliopoteza maisha wakihudumu kwenye sehemu ya mizozo ambapo tuzo ya juu zaidi ya Mbaye Diagne imekabidhiwa kwa

Sauti -
9'55"

22 Mei 2019

Je wajua kampuni zenye viongozi wa ngazi ya  juu wanawake na wanaume hupata faida zaidi?

Sauti -
11'51"

20 Mei 2019

Je wajua kuwa bila nyuki uhakika wa chakula duniani uko mashakani? Hii leo ikiwa ni siku ya nyukia duniani tunakukutanisha na wabobezi kufahamu nyuki na faida zake.

Sauti -
12'3"

17-05-2019

Jaridani Mei 17 , 2019 na Assumpta Massoi

Katika habari kwa ufupi habari ikiwmeo-

-Mashirika ya Umoja wa Mataifa leo yamelaani mashambulizi ya anga yaliyofanyika jana Alhamisi kwenye mji mkuu wa Yemen, Sana'a.

Sauti -
9'55"

16-05-2019

Jaridani Mei 16 na Arnold Kayanda pata habari ikiwemo:

-Mtoto 1 kati ya 7 duniani kote huzaliwa na uzito mdogo kupindukia- Ripoti

Sauti -
12'7"