Jarida la Habari

31 Desemba 2018

Jarida letu la kufunga mwaka hii leo ni mkusanyiko wa matukio  ya mwaka ukiletwa kwako na Siraj Kalyango na Grace Kaneiya. Hata hivyo kuna muhtasari wa habari muhimu hivi leo ikiwemo uchaguzi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Sauti -
9'55"

28 Desemba 2018

Jaridani hii leo na Siraj Kalyango tunaanza na Sudan ambako  yaripotiwa maelfu ya watu wanaandamana kupinga ongezeko la bei za bidhaa sambamba na uhaba wa chakula na mafuta ya gari.

Sauti -
11'44"

27 Desemba 2018

Jaridani hii leo tunaanzia huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako tathmini inaonyesha kuwa mwaka 2018 pekee zaidi ya watu milioni 1 walifurushwa makwao kutokana na mzozo nchini humo.

Sauti -
12'31"

26-12-2018

Jaridani hii leo tunamulika harakati za watu wa jamii ya asili nchini Peru kulinda msitu wa Amazon kwa kuwa ndio tegemeo lao. Tunakwenda Somalia kwa mmliki duka mwanamke ambaye ameajiri vijana na kusaidia kusongesha maisha.

Sauti -
12'47"

24 Desemba 2018

Jaridani hii leo na Siraj Kalyango anaanza na taarifa kuhusu wimbi kubwa la Tsunami lililopiga Indonesia, akikujulisha madhara yaliyoripotiwa hadi sasa. Anamulika pia Kenya na harakati za kukabiliana na uchafuzi wa mazingira ambapo kampuni moja imebuni mkaa utokanao na kinyesi cha binadamu.

Sauti -
11'

21-12-2018

FAO na AU zaungana kuondokana na  jembe la mkono Afrika. Mkulima Msomali asema, ardhi imesalia kuwa mkombozi wangu. Msimu wa baridi, madhila zaidi ya wakimbizi wa Syria nchini Jordan.

Sauti -
12'33"

18.12.2018

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya uhamiaji hii leo , Umoja wa Mataifa unasisitiza uhamiaji unaozingatia utu. Leo washindi wa tuzo ya mwaka huu ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa akiwemo Rebeca Gyumi kutoka Tanzania wanakabidhiwa tuzo hizo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Mjini Ne

Sauti -
13'26"

17 Disemba 2018

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Arnold Kayanda anakuletea

-Mkataba wa kimataifa wa wakimbizi kupitishwa leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani

Sauti -
11'54"

14 Desemba 2018

Leo tunaanzia nchini Tanzania hususan visiwani Zanzibar ambako viongozi wa ngazi ya juu wa Umoja  wa Mataifa wamekutana na wanafamilia wa walinda amani 15 wa Tanzania waliouawa huko DR Congo mwaka mmoja uliopita.

Sauti -
12'5"

13 Desemba 2018

Jaridani hii leo Siraj Kalyango anaanzia huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC  ambako moto umeteketeza vifaa vya uchaguzi kwenye mji mkuu Kinshasa, siku chache kabla ya uchaguzi mkuu nchini humo, Tume huru ya Taifa ya  Uchaguzi, CENI yazungumza.

Sauti -
11'40"