Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

© UNOCHA/Priscilla Lecomte

El Niño na janga la tabianchi vyaibua hofu ya ukame Madagascar

El Niño ambao ni mkondo joto, ni hali ya kawaida inayotokea kwenye baharí ikihusisha joto la hewa baharini na wataalamu wanasema unaweza kuvuruga tena kwa kiasi kikubwa mienendo ya hali ya hewa duniani. Hata hivyo dharura ya tabianchi inayosababishwa na shughuli za binadamu zinaongeza ukali na madhara ya El Niño kwa watu na sayari dunia.

Nchini Madagascar, kisiwa ambacho kiko eneo ambamo kimo baharini linakiweka kwenye hatari ya kukumbwa na hali mbaya hewa kupindukia, Umoja wa Mataifa unashirikiana na mamlaka kusaidia taifa hilo kuhimili na kukabili.

Sauti
4'16"
© UNICEF/Eyad El Baba

Msafara wa vyakula Gaza washambuliwa, wapalestina 234 wauawa mwishoni mwa wiki

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayotoa misaada ya kiutu huko Gaza, Mashariki ya Kati, yameripoti kuwa  kuwa msafara wa malori yaliyokuwa yamebeba vyakula umeshambuliwa kwa kombora leo baada ya mwisho wa wiki uliogubikwa na uhasama na mapigano yaliyosababisha kuuawa kwa wapalestina 234, na hivyo kuzidisha mvutano zaidi kwenye ukanda huo.

Sauti
2'4"
UNICEF Rwanda

UNICEF Rwanda inaboresha maisha ya watoto wenye ulemavu wa kusikia

Ruzuku inayotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Rwanda kwenye vifaa vya kusaidia watoto kuweza kusikia vyema imeleta manufaa na kurudisha ndoto za watoto waliokuwa na changamoto ya kusikia. Leah Mushi anatueleza kuhusu mmoja wa watoto wanufaika. 

Huyu ni Pascaline Uwababyeyi mwanafunzi wa shule ya msingi nchini Rwanda anasema kabla ya kupata vifaa vya kumsaidia kusikia vyema alikuwa hawezi kucheza na watoto wenzake kwani hakuweza kuwasikia kile walichokuwa wakisema. Lakini sasa anaweza kucheza nao kwani anawasikia vyema kabisa.”

Sauti
1'47"
UNHCR/L. Godinho

Kamishna Mkuu wa UNHCR akiwa ziarani Ethiopia anasihi wasisahaulike wanaoikimbia Sudan

Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Filippo Grandi akihitimisha ziara ya siku tatu nchini Ethiopia ametoa wito kwa ulimwengu kuwasaidia watu wa Sudan wanaoikimbia nchi yao na kuingia Ethiopia ambayo ni moja ya nchi wenyeji wa wakimbizi na wakimbizi wa ndani wengi zaidi ulimwenguni. 

“Kuna majanga mengine kote duniani. Mengine makali zaidi na mengine yanaongelewa zaidi. Tusiwasahau watu ambao nimezungumza nao waliokimbia vita Sudan. Hawa wanateseka kila siku na wanahitaji msaada.”

Sauti
1'31"
UNHCR Video

Simulizi ya Islam Mubarak: Ndoto yangu ni kurejea nyumbani na kuishi kwa amani

Kutana na Islam Mubarak msichana mwenye umri wa miaka 21 ambaye vita mpya iliyozuka Sudan Aprili mwaka jana ilimlazimisha kufungasha virago na familia yake na kuukimbia mji mkuu Khartoum na sasa amekwama katika kambi ya wakimbizi wa ndani katika jimbo la El-Gedarif, lakini ndoto yake ni kurejea nyumbani siku moja.

Katika kambi ya wakimbizi wa ndani inayosimamiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ni Islam akiwa amekata tamaa kwa kutouona au kuelezea mustakbali wake .

Sauti
2'30"
©UNDP Syria – Zuhir-Al Fourati

Mashamba darasa yaliyoandaliwa na FAO Syria yainua wanawake wafugaji

Na sasa tuelekee Mashariki ya Kati, Leah Mushi anatueleza jinsi mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo FAO na la Mpango wa chakula duniani WFP yanavyosaidia kuinua maisha ya wananchi katika nchi ya Syria.

Mashariki mwa Syria katika mji wa Deir ez-Zor ulioko umbali wa km 450 kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Damascus, mashirika ya UN lile la FAO na WFP yanafanya kila juhudi kuwajengea uwezo na kubadili maisha ya wananchi kupitia miradi mbalimbali.

Sauti
1'42"
© ICJ-CIJ/ Frank van Beek

Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ yaitaka Israeli iepushe mauaji ya kimbari Gaza

Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ hii leo imeamua kuwa Israel lazima ichukue hatua zote za kuzuia vitendo vya mauaji ya kimbari katika mashambulizi yake dhidi ya wapalestina huko, Gaza, uamuzi unaofuatia shauri lililowasilishwa na Afrika Kusini la kutaka Mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa ichukue hatua za awali kwa mujibu wa Mkataba wa kimataifa wa kuepusha mauaji ya kimbari wa mwaka 1948. 

Sauti
2'13"